Je ni nini kilichofanywa baada ya wanafunzi wa GS Kageyo kuandamana ?

Tarehe ya kwanza, mwezi Juni mwaka wa 2016, Wanafunzi ,hasa wakimbizi wa kambi ya wakongo, wanaojifunza katika sekondari ya Kageyo, katika tarafa la Kageyo, wilayani ya Gicumbi, kasikazini mwa Rwanda waliandamana, hao wanafunzi walikuwa wakilalamika walimu wao takriban 17 waongezwe mshahara na warudishwe kazini baada ya kupelekea uongozi mabarua ya kujiondoa kazini.

Wakiandamana, wanafunzi walivunja madirisha halafu wakashuka mitaani, ambapo askari wa Polisi alitumia risasi mbili kwa kusitisha hayo maandamano.

Makuruki.rw ana habari isemayo kwamba baada ya walimu kuandika mabarua wakisema kwamba hawakutarudi kazini kamwe, uongozi wa shule hiyo uliamua kuajiliwa wengine ingawa hao walimu waliojiondoa kazini waliendelea kuchochea chuki katika wanafunzi wanaotoka kambini kwa kukataa kukubali walimu wapya.
Akiongea nasi, mwanafunzi mmoja alisema kwamba hivi sasa masomo anaendeka.

Yeye alisema ‘’mambo ni shwari, tunasoma vizuri, tumesha sahau hali ya maandamano na walimu wapya wanatufundisha vizuri.’’

Mwanafunzi mwingine naye alithibitisha kuwa hivi sasa wanajifunza hewani ya utulivu.

Na pia Mkurugenzi wa sekondari hiyo Anastase Kamizikunze ametuambia kwamba hewa ya sasa ni kama hewa iliyopo zamani kabla ya wanafunzi kuandaman na pia uongozi umesha jaza nafasi zilizoachwa wazi na wale walioamua kujiuzulu.

Mkurugenzi huyo aliambia makuruki.rw kwamba wao wamesha jaza nafasi 17 za walimu walioacha kazi, 6 miongoni mwao ni wanyarwanda, wengine 11 ni walimu wanaotoka kambini ya wakimbizi ya Gihembe wakati hao walimu 17 wote walikuwa wakongo kabala ya maandamano.

Tuwakumbushe kwamba baada ya maandamano, walimu watutu walitiwa nguvuni wakituhumiwa kutia chumvi mgomo wa hao wanafunzi.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments