Gasabo : wanahangaikia watoto wao wanaokwenda kusoma mbali

Gahakwa Alexandre
Raia wa kijiji cha Gisagara, Tarafa la Gisagara, Wilayani Gasabo wanasema kwamba wanahangaikia watoto wao wanaofanya safari ndeeefu sana kwenda shuleni.
Gisagara ni miongoni mwa vijiji vya tarafa la Gikomero, hasa ni mojawapo wa vijiji vinavyopakana na Wilaya ya Gicumbi kasikazini mwa Rwanda.

Watoto wanaosoma mashule ya msingi husafiri kwa miguu zaidi ya kilomita 7 kwa kufika shuleni. Hiii ndiyo hiyo sababu, wazazi wao wanasema kwamba serikali inapaswa kukumbuka kuwaletea huduma za kielimu karibu yao.

Raia mmoja anayeitwa Gahakwa Alexandre akiongea na makuruki.rw alisema ‘’watoto wetu wanafanya safari ngumu ya kilomita saba kwa miguu kufika Kibara au Gikomero, watoto wetu wanachoka kabisa.’’

’’ tunahangaikia watoto wetu , tunahofu kuwa siku moja tu wataanguka katika mto kwani wao hupita kwenye daraja njiani kwelekea shuleni, nililalamika tatizo hilo tangu Musoni Protaisa alikuwa madarakani, kuikweli, tunahitaji jengo la shule ya msingi hapa.’’ raia alifafanua

akiongea na Makuruki.rw, Katibu mtendaji wa Gikomero. Bwana Jonas amethibitisah ujulikanao wa tatizo hilo, na pia amesisitiza kwamba uongozi unaenda kutatua tatizo hilo mwaka huu wa 2016-2017.

Alisema ‘’Sisi tunajiandaa kuwajengea anagalau madarasa manne mwanzoni, halafu mwaka ufuatao tutajenga madarasa mengine mawili.

Shema Jonas

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments