Maamuzi ya Lionel Messi baada ya kukosa World Cup na Copa America

Nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi mtandao wa 90min.com unaripoti kuwa staa huyo ametangaza kustaafu kuichezea timu yake ya taifa ya Argentina kufuatia kukosa kutwaa taji lolote katika fainali tatu akiwa kama nahodha wa kikosi hicho.

Messi alikosa Kombe la Dunia 2014 katika hatua ya fainali dhidi ya Ujerumani na kukosa Copa America 2015 na 2016 dhidi ya Chile.

“Ni mwisho kwangu kuitumikia kucheza timu ya taifa, sio kwa maamuzi yangu binafsi tu lakini hii inatokana na kukosa Kombe katika fainali nne, Ubingwa ni kitu ambacho nilikuwa nakihitaji zaidi lakini hakikutokea, kiukweli inaumiza kukosa Ubingwa”

Baada ya mechi Messi anatajwa kuwa aliongea na TyC Sport ya Argentina na kueleza kufikia maamuzi hayo, hata inatajwa kuwa sio Lionel Messi pekee aliyetangaza maamuzi hata Sergio Aguero alithibitisha kuwa kuna nyota mwingine atatangaza kustaafu ambaye vyombo vya habari wanaripoti kuwa ni Javier Mascherano.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments