Kanisa la Kikatoliki : Jubilei ya mapadri yazua gumzo mitandaoni

Mwaliko uliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, usemekana kuwa ulichapwa na kanisa la Kikatiloki nchini Rwanda, mwaliko huo ulionyesha orodha ya mapadri wanaotarajiwa kufanyiwa jubilei ya miaka 25 tangu kupewa majukumu ya kiuhuni.

Lakini kitu kilichozua matata ni kwamba wapo kwenye karatasi, mapadri kama Joseph Ndagijimana aliyekuwa padri mkuu wa parokia ya Byimana wakati wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi , Padri Emmanuel Rukundo ambaye alikuwa askari wa jeshi la EX-FAR mwenye cheo cha jemadari na inasemekana kuwa alishiriki kumuua padre mwenzie Mpuguje, wote hao walihusika na uhalifu wa mauaji ya kimbari na kuhukumiwa miaka katika jela na mahakama husika.

Wanyarwanda wengi wakiwemo manusura ya mauaji ya kimbari 1994, watafiti na hata wanasiasa kupitia mitandao yao ya kijamii wanadai kwamba dini ya Katoliki kuadhimisha jubilei ya mapadri wakiwemo na wale waliohusika na ufalifu wa mauji ya kimbari ni kosa la kukana mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka wa 1994.

Katika mahojiano nasi, katibu mtendaji wa tume ya kukabiliana na mauaji ya kimbari nchini CNLG, Dkt Bizimana Jean Damascene alisema wamba aliona hilo tangazo kupitia WatsAp ingawa hajaelewa vizuri.

Alisema “ Mshitakiwa wa mauaji ya kimbari haifai kufanyiwa sikukuu. Jubilei ni siku ya furaha kwa mtu aliyetimiza majukumu yake kwa amani na utulivu. Hatuelewi jinsi mtu aliyehukumiwa kifungo cha miaka Fulani anaweza kupongezwa, uhalifu wa mauaji ya kimbari ni dhambi kubwa kuliko dhambi zote. Tutaongea na dini la Kikatoliki kuhusu jambo hilo tukiwa pamoja”.

Makuhani wengine watakaoadhimisha jubilei ya miaka 25 ni Lukanga Kalema Charles, Rutarema Rukanika Aime, Gatete Theotime, Rubasha Zirimwabagabo Emmanuel, Rukundo Emmanuel, Uwigaba Jean Baptiste.

Askofu Mbonyintege akiongea na igihe.com, Yeye amepuuzilia mbali tangazo hilo, amesema hajui watu waliofanya orodha yaani wana lengo lao la kipekee.

Alisema “Sikufanya orodha hiyo, ni watu wanaotaka kuchafua sifa yetu, makuhani watakaofanyiwa jubilie ni wale unaona kwenye orodha hiyo, wale wanaofungwa wakihusika na hatia ya mauaji ya kimbari hakufanyiwi sikukuu”.

“Katika orodha mliopewa, mapadri wakayefanyiwa sikukuu ni wale waliopewa majukumu katika mwaka wa 1991, Jubilei itafanyiwa wale ambao bado tuko pamoja hapa Kabgayi si jubilei ya mapadri waliohukumiwa uhalifu wa mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka wa 1994. Askofu Mbonyintege aliongeza.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments