Gasabo : Raia wanaombwa kuwa wa kwanza kulipa bima ya kiraia.

Jana ilikuwa Juni, tarehe ya 25 mwaka wa 2016, siku ya kufanya UMUGANDA, wananchi waliotoka vijijini vya Munini na Murambi, Wilyani ya Gasabo, tarafa la Gikomero ambapo wao walijijengea barabara ambayo inayokwenda kitovu cha ufundi ‘’AGAKIRIRO ‘’ ambacho kinategemewa kufunza angalau watu 200.

Akitoa hotuba, Murugande Benjamin makamu kiongozi anayeshughulikia maswala ya kijamii, aliwakumbusha raia kwamba ni vyema kulipa bima ya kiraia MUTUELLE DE SANTE mapema na wale wasio kipato wakasaidiwa kulipa bima yao.

Alisema ‘’hatataki mtu kutesekea nyumbani kwa sababu ya kutotoa MITUELLE DE SANTE, tunataka nyinyi mshirikiane, mkashindwa, muombe uongozi kuwasaidia.’’

Bi.Gafaranga Brigitte, katibu wa kikao halmashauri cha mji wa Kigali akitoa hotuba
Katibu wa kikaao halmashauri wa mji wa Kigali Bi. Gafaranga Brigitte aliwaomba raia kuongeza nguvu kwani mwaka jana walishindwa kushika nafasi nzuri kwenye orodha ya waliolipa bima kwa idadi kubwa , Yeye aliwaomba kujipia bima kwa idadi kubwa ili wawe wa kwanza mwaka huu wa 2016-2017.

Alisisitiza ’’tafadhali !, mlipe haraka, mwaka uliyopita mlichika mkia, mwaka usoni, nataka nyinyi mshinde, nataka kushereheka hapa kombe la watu waliolipa MITULLE DE SANTE.’’

Mwaka huu, bima ya kiraia MUTULLE DE SANTE, Wizara ya mamlaka ya ndani iliamua kwamba Bima itapewa kutoka na viwango vipya vilivowekwa na wizara hiyo kutokana na kipato cha kila familia.

Siku ya jana, raia wa Gokomero walijitengea barabara yenye urefu wa 24400 na ya thamani ya 5,100,000. Faranga za Kinyarwanda.


wakiwa na viongozi, wao walijitengea barabara

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments