Nyagatare : Ashtakiwa utumiaji wa pesa feki

1

Jeshi la polisi katika jimbo la mashariki wilayani Nyagatare limemshika Nsengiyumva Jean Claude mwenye umri wa miaka 28 pia mfanyakazi wa kituo cha afya cha Karangazi ambaye hushtakiwa kutumia pesa feki na kuzipa mfanyakazi wa huduma za Mobile Money.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoawani Mashariki IP Emmanuel Kayigi alisema” Nsengiyumva alikuja katika masaa ya usiku kwa lengo la kutia pesa elfu thelathini (30.000 Frw) kwenye nambari yake ya mobile money lakini mwenye kutoa hudumu alikuwa na wasi wasi ya pesa hizo alizopewa punde si punde alipochunguza vizuri ndipo alipoona kuwa alipewa pesa feki. Aliamua kutuambia kisha tukaenda nyumbani kwake ndipo tulimkuta akiwa na pesa feki elfu ishirini kitandani mwake".

Nsengiyumva anasema kuwa hakuwa kuwa pesa hizo ni feki kwani alizipewa na mwenzie kama malipo ya deni.

IP Kayigi alipongeza mfanyakazi huo wa huduma za Mobile money na kutoa ushauri wa kuandika vitambulisho vya kila mtu kabla ya kutoa huduma ili wakati wa tukio kama hili iwe rahisi kukamatwa kwa mhusika bila kusahau kuchunguza vizuri wakati wa kutoa huduma na kuangalia kwenye akaunti zao ili kuhakikisha idadi ya pesa zinazobaki baada ya kuondoka kwa yule aliyepewa huduma.

Nsengiyumva anafungiwa kwenye kituo cha polisi cha Karangazi wakati upererezi unapoendelea. Kitabu cha sheria kunaandikwa kuwa mtuhumiwa wa utumiaji wa pesa feki huhukumiwa kifungo cha miaka miwili hadi miaka mitano na faini ya pesa kuzidisha mara mbili kadi kumi za pesa feki alizozitumia.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments