Msimamo wa uchaguzi barani Afrika

1

Uchaguzi ni njia ya msingi ya jamii ya kujipatia viongozi kidemokrasia. Sifa mojawapo ya uchaguzi wa kidemokrasia au wa huru na haki ni uchaguzi kufanyika kwa siri. Sifa nyingine ni uchaguzi kufanyika mara kwa mara katika vipindi vinavyoeleweka, uchaguzi kutoa fursa sawa kwa wagombea wote, na uchaguzi kuruhusu waangalizi wa ndani na wa nje kuwafuatilia.

Katika Afrika kuna mifano wazi wakati wananchi wanaposema kwamba hakuna uchaguzi wa kidemokrasia uliofanyika yaani wizi wa kura, rushwa na udanganyifu na wanaona kuwa ni kupoteza wakati na fedha kufanya uchaguzi barani Afrika.

Hatuwezi kusahau kuwa kuna baadhi ya nchi barani Afrika uchaguzi unapofanyika kwa njia ya amani, kidemokrasia, bila udanganyifu na wizi wa kura ingawa ni mara chache.

Kwa hiyo, unapofika uchaguzi mwingine chama tawala kinakuja tena na ahadi zile zile za kuwaletea wananchi maji, elimu bora, huduma bora za afya, barabara na kadhalika.

Katika mazingira hayo ya kurudiwarudiwa ahadi zile zile, wananchi hutambua kwamba chama tawala kinawadanganya na kinachezea akili zao. Kwa hiyo, hujipanga kukichagua chama cha upinzani.

Chama tawala kikitambua kuwa wananchi wamejiandaa kukitoa hutumia mizengwe, rushwa, na wizi wa kura kwa kutumia tume za uchaguzi. Mwisho wa siku wananchi wanatangaziwa ushindi wa chama tawala. Matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi yanaathiri vyama visivyo na uwezo mkubwa wa kifedha na wagombea wasio na uwezo mkubwa wa kifedha.

Halafu kuna suala la kutumia nguvu kubwa na Serikali kudhibiti wapinzani wasishinde uchaguzi. Utakuta Serikali ya chama tawala inatumia polisi kudhibiti wapinzani wasifanye mikutano, wasiandamane, na washinde kwa mbinde.

Maeneo ambayo wapinzani wanakuwa wapole wanaporwa ushindi. Kinachotakiwa ni mgombea aliyeshinda kutangazwa mara moja kuwa ameshinda bila kusubiri zitokee vurugu. Jambo jingine linalovuruga chaguzi barani Afrika, ni kunyanyaswa wapinzani kwa lengo la kuwakatisha tamaa ili wasigombee tena katika chaguzi.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments