Polisi Rwanda yaonya watu ambao wanachukua picha wakati wa ajali

1

Sp Jean Marie Vianney Ndushabandi
Polisi ya Rwanda inawaonya watu wanaofurahishwa na kuchukua mataswira bila ruhusa wakati wa ajali halafu wakaanza kuyasambaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba watu kama hao wanaweza kuadhibiwa.

Katika mkutano kielimu kwenye kiwango cha mji wa Kigali uliyofanyika Mwezi Juni, 23 mwaka wa 2016, Msemaji wa polisi inayoshughulikia usalama wa kitaani Sp Jean Marie Vianney Ndushabandi wakati alikuwa kutoa hotuba kuhusu tatizo la watoto barabarani wakienda au wakitoka shuleni,
amesema kwamba watu wanapaswa kuachana na desturi ya kusamabaza kwenye mitandao ya kijamii picha walizochukua mahali ambapo ajali iliyotukia.

alieleza kwamba wakati wa ajali watu wanaweza kuwa makini kwamba wa kutotuma picha zinazoweza kusababisha kiwewe au picha zinazoonyesha unyanyasaji.

alisema ’’Kifo ni jambo la kawaida ikiwa kifo kinachosababishwa na ajali au maradhi, ukichukua picha ya mzazi kabla ya polisi kufika kisha ukaanza kuyasambaza kwenye mitandao ya kijamii, nadhani hii ni hatua ya unyanyasaji.’’

aliedelea kusema kwamba kuheshima ni desturi ya Kinyarwanda, mfu au mtu hai anaweza kuheshimika.

Kila mtu atakayehukumiwa kusambaza picha za aina hiyo atapewa adhabu inayomfaa.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments