Viongozi wa mashirika ya michezo wameogopa Maseneta.

Tume ya maseneta wanaoshughulikia masuala ya kijamii, haki za kibinaadamu Bungeni la Rwanda walikuwa kualika vyama vya michezo kwa ajili ya kuzungumzia maendeleo ya spoti nchini Rwanda, Lakini hakuna mtu aliyeshuhudia mwaliko huo kwenye saa iliyosemwa katika barua pepe ambayo ilitumwa kwa wakuu wa mashirika.

Mazungumzo alitarajia kuanza saa tatu za asubuhi katika chumba cha maseneta lakini mwandishi wa makuruki.rw aliyefika huko dakika chache kabla ya saa tatu, aliwana maseneta wakisimama nje ya chumba.

Maseneta waliendelea kungoja wanachama wa mashirika lakini hakuna mtu aliyekuja bungeni. Kisha maseneta waliamua kuahirisha mazungumzo.

Mkuu wa tume hiyo ya maseneta, Seneta Niyongana Callican amesema kwamba waliwatumia mwaliko, lakini licha ya kutohudhuria majadiliano, wataendelea kujadiliana na wizara ya michezo na utamaduni Rwanda.

Alisema ‘’nasi hatujui sababu iliyowafanya kutohudhuria, lakini tunajua kiuhakika kwamba walipokea mwaliko wetu.’’

Baada ya mazungumzo kuahirishwa, Mwandishi wetu amekutana na mkuu shirika la sataranji na akiwa pamoja na mkuu wa shirika la wa tenisi nje ya chumba, Wao wanasisitiza kuwa wao wamechelewa kufikiwa na barua pepe.

Ganza Kevin. mkuu wa shirikisho la mchezo wa Sataranji
Ganza Kevin mkuu wa shirika la sataranji, mmoja wa waliochelewa, amebaini kuwa ingawa ya kuchelewa, Yeye amekuja licha ya kuahirishwa kwa mazungumzo.

Alisema’’ ndio, tulipokea barua pepe, nimekuja, hata kama maseneta wameamua kuahirisha mazungumzo, nadhani tutakutana upesi.’’

Semigabo Fulgence, aliyewakilisha shirika la tenisi (table tennis)
Semigabo Fulgence mwakilishi wa shirika la mchezo wa tenisi (table Tenis) , Yeye amesema kwamba amekelewa kwa sababu ya wapekuzi kwenye mwingilio wa jengo la Bunge waliompekuwa muda mrefu.

Tume hii imesema kwamba waliwatumia viongozi wa mashirika ya michezo mwaliko kwa ajili ya kujadiliana kiwango cha michezo nchini Rwanda na kuungana mkono kwa kuendeleza michezo.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments