Rais Kagame na Rais Déby wamezungumzia Maandalizi ya mkutano wa AU.

Rais Paul Kagame wa Rwanda amemkaribisha mwenzake kutoka Jamhuri ya Tchad na pia mkuu wa umoja wa Afrika Mheshimiwa Idriss Deby Itno, jana Juni 22,2016 baada ya Rais Itno kutua uwanja wa Ndege Kanombe katika saa za asubuhi.

Uwanjani wa Ndige, Yeye alipokelewa na Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano Louise Mushikiwabo, Mkuu wa Jeshi la Rwanda Jenerali Patrick Nyamvumba na mkuu wa polisi ya Rwanda IGP Emmanuel K. Gasana.

Rais Kagame na Deby wamejadiliana maandalizi ya kongamano la AU litakalofanyika Nchini Rwanda mwezi ujao Julai tangu tarehe 10 hadi 18 mwaka huu.

Rais Deby jana katika saa za alasiri alirudi kwake Nchini Tchad baada ya kukamilisha ziara ya ya siku moja rasmi nchini Rwanda.

Mapema, Dk Nkosazana Dlamini zuma(mkuu wa tume ya umoja wa Afrika) alitembelea Rwanda akilenga kujionea macho kwa macho maandalizi ya kongamano hilo.
Dk zuma alipongeza Rwanda kwa maandalizi mazuri na pia alisema kwamba yeye anadhani kuwa wao wataonja msisimuko wa hayo maandalizi mazuri yenye ubora wakati wa mkutano.

Waziri Louise Mushikiwabo wa mabo ya nje na Ushirikiano na Rais Paul Kagame wakimkaribisha Rais Idriss Deby

Rais Paul Kagame wa Jamhuri ya Rwanda akimtakia Deby safari njema baada ya ziara yake ya siku moja nchini Rwanda

Habari nyingine ambazo zina uhusiano na ziara ya Rais Idriss Deby Itno wa Tchad nchini Rwanda.
http://sw.makuruki.rw/spip.php?article2489

http://sw.makuruki.rw/spip.php?article2492

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments