Wafanyakazi wa Wilaya ya Gasabo wakimbilia ofisi zao.

Katika masaa ya saa nane za mchana, wafanyakazi wa Wilaya ya Gasabo mjini Kigali wamekimbilia vikali ofisi zao kutokana na fununu ya moto.

Hao wafanyakazi walianza kukimbia baada ya kusikia chombo kinachotumiwa kwa kuhesabu nguvu za umeme (Cash power) kulipuka.

Mfanyakazi mmoja aliyezungumza na makuruki.rw alisema kwamba watu walikuwepo ofisini walianza kukumbia nje ya ofisi kwa hofu ya kuteketezwa.

Lakini mashuhuda wamesema kwamba, kwa ushirikiano na polisi, taasisi ya umeme Rwanda na raia walikuwepo hapo walisaidiana kuizima moto kabla ya kuanza kuwasha jengo hilo.

Jengo la wilaya ya Gasabo liliyopo maeneo ya Kacyiru mbele ya Balozi ya Marekani Nchini Rwanda.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments