Wabunge wahangaikia uhaba wa makaburi katika makambi ya Wakimbizi.

Ripoti iliyotolewa na tume ya wabunge wanaoshughulikia mambo ya nje na ushirikiano katika Bunge la Rwanda kuhusu safari waliofanyia katika makambi ya wakimbizi tangu mwezi Machi, tarehe 07 hadi 12, 2016, Katika Ripoti hiyo, wabunge walionyesha kwamba wakimbizi wana matatizo kadhaa yakiwemo uhaba wa makaburi katika makambi ya wakimbizi ambapo wafu wanasongamana vikali kwenye eneo ndogo la kaburi.

Wabunge ambao walikwenda kukagua makambi , wanasema kwamba walikuwa nia mbalimbali ikiwemo kujua sababu kiukweli ya kuongezeka kwa idadi ya wakimbizi wanaokimbilia Rwanda wakitoka nchini zao, matatizo wanokabiliwa, na kuchumbua ikiwa wakimbizi hawathiri mazingira ambapo wanapoishi.

Miongoni mwa matatizo yaliyojitokeza katika makambi yote ni uhaba wa chakula, kuni, unyanyasaji ambayo hufanyiwa wanamke na watoto, vijana wasio na kazi na kadhalika.

Mkuu wa tume ya hao wabunge Mutimura Zeno alisema kwamba wao waliteketezwa mioyo na uhaba wa makaburi katika makambi ya wakimbizi. Hususan kambi ya Wakongo.

Alisema ‘’uhaba wa makaburi hasa katika kambi ya Kigeme(kambi ya Wakongo) ambapo wafu wakumbwa na mafuriko, tunaogopa kuwa hatakuwepo muda mvua ikanyesha halafu wafu na watu hao wakakumbwa na mafuriko katika kinamasi, lakini tulijulisha MIDMAR kwamba hilo ni tatizo hatari.’’

Kingine ni kwamba wapo wakimbizi wanaotaka kwenda Marekani kasha wakaanza kugawanya wenzao ili kusababisha vurugu kama dalili isemayo kwamba hawana usalama mahali wapo.

Wabunge walieleza kwamba tatizo la wakimbizi wakongo haiwezikane kutatuliwa wakati wowote tatizo la waasi wa FDRL wanaoishi misituni ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hakuchukuliwa uamuzi sahihi.

Mbunge Ruku Rwa Byoma alisema ‘’tunasema mikutano ya kimataifa, na pia tunasema mikutano ya Ukanda, tunajua tatizo, lakini hatuoni suluhu la kuitokomeza FDRL.’’

Hao wabunge walizuru makambi ya Kigeme, Kiziba, Mahama, Nyagatare, Bugesera, Nyabiheke, Nkamira na Gihembe.

Hivi sasa, nchi ya Rwanda ni kimbilio la wakimbizi zaidi ya 162,254 wakiwemo Wakongo, Warundi na wengine.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments