Kagame aipigia saluti Cleveland Cavaliers

Rais Paul KAGAME alikuwa akishabikia Golden state warriors ambayo iliyonsehwa kivumbi na Cleveland Cavaliers ya Lebron James aka King James
Siku za hivi karibuni Raisi Paul Kagame wa Rwanda amejitokeza kuwa shabiki wa timu ya kikapu ya Marekani Golden state warriors. Lakini baada Golden State warriors kulazwa na Clevland Cavaliers jijini la Oakland/California huko Marekani, Kagame amekubali kuchapwa .

Katika usiku, tarehe 19 mwezi Juni mwaka 2016 Cleveland Cavaliers imewabamiza Golden state warriors vikapu 93 kwa 89 ambapo LeBron James aka King James ameibuka nyota wa mechi hiyo.

Baada ya kushindwa Rais Kagame amewapongeza mno Cleveland Cavaliers na wachezaji hususan Lebron James

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Kagame amesema eti ‘’isipokuwa Ange KAGAME , ndiye alijaribu kushabikia Cavs, lakini nae alishabikia wote wawili Cavs asilimia 60 na Golden stste warriors asilimia 40.’’

Raisi Kagame aliendelea kusema kwamba kushinda si bahati, Ushindi unapatikana kwa watu ambao wanaofaa kushinda

Kagame anajulikana kuwa shabiki wa michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu ambapo Yeye ni shabiki wa washika bunduki ‘’Arsenal ‘’ya Premier League huko Uingereza.

Janvier KARANGWA
@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments