Je kuna Udikteta hupigania maslahi ya Taifa ?

Kuna watu wanaotafsiri udikteta kwamba kiongozi anayekaa madarakani kwa muda mrefu ndio dikteta wengine husema kwamba raisi anaeongoza nchi kwa sheria kali ndio dikteta. Na vilevile wengine wanaona kiongozi anayeua na kuweka amri kama za kijeshi ndio dikteta.

Udikteta ni hatari sana kwa sababu mwananchi atakosa uhuru wake katika maisha yake na kumnyanaysa haki za kibinaadamu. Kiongozi atakuwa na uwezo wa kumiliki nchi pamoja na mali zote za nchi.

Dunia inawakumbuka sana madikteta waliowahi kuvuma miaka ya 1930 hadi 1950 kama akina Adolf Hitler wa Ujerumani na Joseph Stalin wa Soviet Union. Wote hawa wanajulikana kama madikteta waliowahi kuogopewa na kuvuma ndani na hata nje ya nchi zao.

Hitler alikuwa dikteta mshenzi na mbaya kuliko wote duniani kwa vile aliufanyia ulimwengu ukatili wa hali ya juu kwa maslahi ya kuifurahisha nafsi yake na kukamilisha imani yake kwamba binadamu bora duniani ni Mjerumani peke yake na wengine wote wanastahili aidha kuuwawa au kuwa watumwa wa Wajerumani.

Joseph Stalin alikuwa dikteta aliyeogopewa kwa kulinda kauli na msimamo wake kwa maslahi ya taifa lake. Je, ni kwanini tunatakiwa tuamini kwamba kuna madikteta wazuri na wabaya.

Dikteta mbaya ni yule anayetunga sheria na kuweka taratibu zenye makusudi ya dhati ya kumuongezea madaraka na mamlaka makubwa kwa madhumuni ya dhati ya kuwagandamiza wananchi wake na huku akijinufaisha yeye mwenyewe na familia yake na wale wote waliomzunguka na wanaomshabikia kwa yale yote anayoyafanya ?

Dikteta mzuri ni yule anayetunga sheria na kuweka taratibu zenye makusudi ya dhati kuliletea taifa maendeleo makubwa kwa kuzingatia kwamba Serikali inatenda haki kwa kila raia ; na kuhakikisha kwamba kila raia ananufaika sawa na wengine na huduma za umma, haki za kiraia na kupata mgawo sawa wa pato la taifa bila ya kujali elimu yake, kabila lake, dini yake, umri wake, sura yake na rangi yake ?

Nyaraka za Dkt. Noordin Jella

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments