Mtuhumiwa uchinjaji atiwa nguvuni Gicumbi

Theoneste Mugabo alichinjwa katika usiku wa tarehe 16 mwezi Juni mwaka wa 2016
Jana, tuliandika habari iliyosema kwamba wilayani ya Gicumbi mnusura wa mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 dhidi ya Watutsi aliuawa. Mugabo Theoneste alikatwa shingo na watu wasiojulikana nyumbani kwake.

Lakini leo asubuhi katibu wa tarafa la Bukure aliambia mauruki.rw mtu anayetuhumiwa kumua Theonesta amesha kamatwa.

Nsabimana J.Damascene ametiwa nguvuni kwani baada ya marehemu kuchinjwa alikuwa nae saa za jioni kabla yeye kuchinjwa saa za usiku.

Katibu wa tarafa hilo, Rusizana Joeph amesema kwamba Nsabimana J.Damascene anadaiwa kwamba ikiwezekana kuwa Yeye anahusika na kifo cha Theoneste, anadaiwa kumua akitaka kumnyakua pesa zake marehemu alizopata baada ya kuuza shamba lake kwa kujipanga kufanya ukarabati wa nyumba yake.

Hivi sasa, Nsabimana amewekwa kwenye stesheni ya Polisi huko Bukure, Wilaya ya Gicumbi Kasikazini mwa Rwanda.

Janvier KARANGWA@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments