Mamlaka ya mapato Rwanda kuwapa wanunuzi gari kwa bure.

Ruganintwari akieleza mpango wa IZIHIRWE
Mamalaka ya mapato Rwanda RRA imewaletea wanunuzi mpango mpya ‘’IZIHIRWE’’ unayolenga kupa mtu gari kwa bure, RRA inawaomba wanyarwanda na hata wageni kuomba risiti inayotolewa na EBM baada ya kununua kila bidhaa wanazonunua.

Uongozi wa RRA unasema ni kwa kuhamasisha watu kuomba risiti hiyo ya EBM(Electroni Billing Machine), kuhamasisha wauzi kutumia mfumo wa EBM na hata kumpongeza yeyote aliyeomba bili ya EBM.

Kamishna mkuu wa RRA, Ruganintwari Pascal, katika mahojiano na wanahabari
alisema ‘’ sasa, IZIHIRWE inalenga kuhamasisha wauzi na wanunuzi kutumia mfumo huo wa EBM, wanunuzi tumewaletea nafasi za kuwapeleka kileleni, mnunuzi akiomba risiti, moja kwa moja atakuwa nafasi ya kushindia tuzo za kumckekesha.’’

Aliendelea kusema kwamba wanunuzi hao watapewa tunzo kadhaa zikiwemo pikipiki, runinga, na Gari.

Kitu sahihi ambacho Mnunuzi anatakiwa kufanya, ni kuandikisha risiti yake akitumia simu yake ya mkononi kwa kupiga *800# kisha akazingatia vigezo na masharti.

kumbuka, wewe unaweza kumiliki gari, pikipiki, na hata runiga

Janvier KARANGWA@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments