Gicumbi : Mnusura wa mauji ya kimbari amechinjwa

Leo asubuhi tarehe 17,Juni mume anayeitwa Mugabo Theoneste mwenye umri wa miaka 48 ameuawa akikatwa shingo na watu bado hakujulikana.

Mugabo Theoneste ambaye alinusurika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi, ambaye aliyeishi Wilayani ya Gicumbi, tarafa la Bukure, kijijini cha Karenge, maeneo ya Nyarutovu ;.

Habari kuhusu kifo chake amejulikana kwa mara ya kwanza akitangazwa na shangazi yake Mukaminega Dansilla.

Dansilla ametangaza kwamba alimngoja marehemu ili amsaidie kazi katika mgahawa lakini Theoneste akachelewa kuja, Dansilla amendelea kusema kwamba amejaribu kumpigia simu mara nyingi bila kumpata kwenye line halafu Yeye alienda kumtafuta nyumbani kwake.

Amesema ‘’saa 7 na dakika 10 za asubuhi ndipo nimefika nyumbani kwake, nilishangaa kuona mlango wazi kisha niliingia ndani nikamuona akilala kitandani, nikisogea mbele nikatambua amekatwa shingo na panga amabayo wauaji walitumia kumkata shingo nyuma yake kitandani.

Katibu mtendaji wa tarafa la Bukure , Rusizana Joseph ametangazia Mkuruki.rw kwamba uhalifu kama hivi tarafani hilo ni kwa mara ya kwanza kujitokeza.

Tumejaribu kuongea na msemaji wa Polisi katika jimbo la Kasikazini lakini hawezi kupatikana.

Wakati wa kukumbuka mauaji ya kimbari ya mwaka wa 1994 dhidi ya Watutsi mwezi uliyopita wa Aprili kesi zaidi 40 zilipatikana.

Janvier KARANGWA@sw.makuruki.rw

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments