Wafungwa wa1930 kwenda Mageragere siku za usoni.

Gereza ya Kigali maarufu kama Dix neuf cent trente
Taasisi ya huduma za kurekebisha Rwanda RCS imetangaza kwamba wfungwa wanaofungiwa gerezani ya Kigali kwa umaarufu Dix neuf cent trente (1930) kutokana na mwaka ilipojengwa. Taasisi hiyo inasema kuwa miezi mitatu tu ijayo wafungwa wote wataenda kufungiwa katika jela mpya iliyojengwa katika maeneo ya Mageragere, Wilaya ya Nyarugenge.

1930 ni gereza ya kihistoria iliyojengwa katika enzi za kikoloni ambapo iliwasaidia wakoloni kuwadhibu wahalifu .

Hivi sasa RCS inasema kwamba Jela ya Mageragere iko karibu kumalizika Mkuu wa RCS CGP George Rwigamba amesema kwamba wanafikiri kuwachukua wafungwa Mageragere angalau miezi mitatu ya usoni.

Kamishna mkuu Rwigamba amesema ‘’ujenzi wa jela ya Mageragere unafika tamati isipokuwa ufungaji wa bomba la maji bado hakumalizika, na hivi sasa tunaharakisha ujenzi wa nyumba mbili zitakazo kupokea wafungwa wa Jela ya Nyarugenge, nadhani mwezi septemba tutakuwa kumaliza kuhoja wafungwa katika jela hiyo mpya ya Mageragere.’’

Kuhusu maji Rwigamba ameongeza kuwa wao wanazungumza na WASAC kwa kuwaletea maji kwa haraka.

Jela ya Mageragere ikimalizika kujengwa yeye inatarajiwa kupokea wafungwa wote wa jela ya Gasabo na hata ya Nyarugenge ; kutokana na mjibu wa taasisi ya kurekebisha Rwanda RCS.

Hivi sasa Rwanda ana magereza 13 ya watu wakubwa na nyingine moja ya watoto

Kamishna mkuu wa RCS CGP George Rwigamba

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments