Christiano kashindwa kuisaidia ureno

Ureno wamelazimishwa sare na Iceland katika mechi za Euro2016 huko Ufaransa licha ya mastaa wengi kama Ronaldo na Pepe wa Ureno ambao waliotarajiwa kuichapa kirahisi Iceland ; Lakini wametoshana nguvu katika Mchezo uliomalizika usiku kwa Timu hizo kugawana alama kufuatia sare ya bao 1-1.

Ureno ilianza kuzitikisa nyavu za Iceland kwa bao la Luis Nani dakika 31 kipindi cha kwanza, na Iceland wakizawazisha bao hilo kupitia kwa Birkir Bjarson dakika 50 kipindi cha pili.

Gylfi Sigurdsson alipoteza nafasi ya kuipa Iceland bao la kuongoza baada ya shuti lake kuokolewa.

Mpira wa kichwa uliopigwa na Cristiano Ronaldo uliokolewa dakika za lala salama huku Iceland wakikaribia nao kupata bao la ushindi lakini mkwaju wa Alfred Finnbogason uliokolewa.

Iceland walikuwa wanacheza mchezo wao wa kwanza wa mashindano makubwa, licha ya Ureno kumiliki mpira kwa asilimia nyingi lakini hawakufanikiwa kuchomoka na ushindi.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments