Urusi kupigwa marufuku kutoka Euro 2016

Urusi huenda ikapigwa marufuku ya kushiriki mechi za Euro za mwaka 2016 kutokana na fujo zilizosababishwa na mashabiki wake siku ya Jumamosi wakati wa mechi kati ya Urusi na Uingereza mjini Marseille.

Mafisa wa shirikisho la kandanda barani ulaya, UEFA, pia wameipiga Urusi faini ya euro 150,000.

UEFA ilisema kuwa adhabu hiyo itatekelezwa ikiwa ghasia kama hizo zitatokea tena katika mechi za Urusi zilizosalia.

Makundi ya mashabiki wa Urusi wanasafirishwa kutoka Ufaransa baada ya kushuhudiwa visa kadha katika mechi ya Euro mwaka 2016.

Urusi pia imedhibiwa kwa visa vinavyohususu ubaguzi wa mashabiki na ufyatuaji fataki wakati wa mechi.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments