Sura Mpya ya Ugaidi Nchini Rwanda

Waziri wa usalama wa Rwanda, Musa Fazil Harerimana alielezea wabunge kuwa tatizo la ugaidi limechukua hatua mpya, lakini serikali inashiliakiana na shirika la waislamu (AMUR) ili kutafuta sururuhisho la tatizo hilo kwani laweza kuharibu vitu vingi ikiwemo usalama wa nchi.

Wakati waziri wa usalama alipowasilisha bajeti ya mwaka kesho , makamu rais wa mali ya serikali Mukayuhi Constance aligusia tatizo la ugaidi na kutaka kujua hukaa kivipi.

Waziri Harerimana alisema kuwa msingi wa tatizo hili ni fikra ya upande mmoja wa washiriki wa dini la kiislamu lakini alionyesha kidole cha shahada watu wanaosema kuwa kuna nchi nyingine waliyoandaliwa kuishimo ambayo haiendani na imani ya kiislamu.

Kuna watu ambao huambiwa kuwa wanaenda kuishi katika nchi ya amani na utulivu lakini wakajikuta katika hali ya utumwa.

Alisema “Kuna watu wanaoulizwa vitambulisho na jeshi la polisi lakini wakasema kuwa walikuwa navyo wakati walipokuwa watumwa wa shetani lakini leo wameokoka utumwa”.

Wale wanoenda katika makundi ya wanamgambo hudanganywa kuwa kuna maisha wasioweza kuishimo, wakafundishwa kukataa dunia na maisha yao kisha wakajikuta katika ugaidi.

Kuna watu wanaosema kuwa wanaishi katika maisha ya ufukara lakini kwa upande wa waziri wa usalama hakubaliani na kauli hii kwani kuna watu waliotajilika lakini unawakuta katika makundi ya ugaidi.

Katika kutatua tatizo hili la ugaidi kunapaswa kushirikiana na shirika la kiislamu katika nchi hizo ili watu hao wakamatwe.

Alisema “Tibu la kudumu, shirika la kiislamu lina majukumu ya kufundisha dini la ukweli isiyo na ubaguzi wowote wala chuki ili walekebishe makosa yaliyofanywa na wenzao”.

Ushirikiano katika familia unapaswa kuwa ngao ya msingi ili kusogelea watoto na kuchunguza vile wanavyofanya kila siku kwa kutambulika.

Tangu Januari 2016 wahatia kadhaa wa ugaidi walikamatwa na jeshi la polisi nchini.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments