Eritrea na Ethiopia zapigania eneo la mpakani

Eritrea na Ethiopia zapigania eneo la mpakani
Eritrea imeishtumu Ethiopia kwa kutekeleza shambulio katika mpaka wake ambao una ulinzi mkali.

Wakazi katika eneo la Tsorona wanasema wamesikia milio ya risasi na kuona wanajeshi wakielekea katika mpaka.

Hata hivyo Waziri wa habari wa Ethiopia amesema hafahamu lolote kuhusu vita hivyo.
Zaidi ya watu laki moja walifariki katika mapigano yaliyodumu mika miwili na nusu katika ya mataifa yote mawili.

Kamati ya Umoja wa Mataifa ilisema kuwa eneo linalozozania linapaswa kuwa la Eritrea, lakini Ethiopa haijawahi kukubali uamuzi huo.
Mwandishi wetu Emmanuel Igunza anasema kuwa wakaazi wa eneo la Tsorona kwenye mpaka wa Ethiopia na Eritrea wanasema kuwa wamesikia milio mikubwa ya risasi kuanzia Jumapili asubuhi.

Pia wameripoti kuwaona wanajeshi wa Ethiopia waliojihami kwa silaha kali wakipita katika mji huo wakielekea maeneo ya mpakani.
Lakini waziri wa habari wa Ethiopia ameiambia BBC kuwa hafahamu lolote kuhusu mapigano hayo.

Eritrea kwa upande wake imetoa taarifa inayoshtumu Ethiopia kwa kuanzisha mapigano hayo.

Nchi hizo mbili zimekuwa na mzozo wa miaka mingi kuhusu eneo la Badme ambalo kamati iliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ilisema inapaswa kuwa ya Eritrea.
Lakini Ethiopia imepinga uamuzi huo ambao hadi kufikia sasa haujatekelezwa kikamilifu.

Zaidi ya watu elfu mia moja walifariki kati ya mwaka wa 1998 na mwaka wa 2000 katika mapigano makali kuhusu mpaka.

Mapigano katika eneo hilo la mpakani yamefanyika awali lakini ni nadra sana.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments