Bajeti mpya ya Rwanda mwaka wa 2016/2017.

Waziri wa mipango na fedha Bw. Balozi Claver Gatete
Waziri wa mipango na Fedha nchini Rwanda, Balozi Gatete Claver amewaelezea wabunge kisia cha bajeti ya mwaka wa 2016/2016. Amesema kwamba bajeti hii itakuwa bilioni 1 949.4 za pesa za Kinyarwanda.

Balozi Gatete amesema kwamba 37.6% ya pesa hizi ndiyo yatakayotoka ugenini, lakini 62.4% zitapokewa nchini Rwanda kutokana na kodi za wananchi. Wazili Gatete amesema kwamba fedda hizi zitatumika kuhusu mambo ya vipaumbele.

Wazili Gatete amesema kwamba kama maendeleo duniani hata barani Afrika yamesogea mbele, hivi vinayiwezesha nchi ya Rwanda kusogea mbele kimaendeleo. Ameongeza akihakikisha kwamba bajeti ijao ya mwaka wa 2018/2019 itapanda kwa kiwango cha 6%.

Hususan, Wazili Gatete ameongeza kwamba bajeti ya mwaka huu imepanda kufika bilioni 140,6 zaidi ya mwaka uliopita wa 2015/2016. Bajeti ya mwaka huu ilikuwa bilioni 1 808.8.

Waziri Gatete amesema kwamba kiwango kikuu cha bajeti ya mwaka huu kitapatikana nchini Rwanda ; hii ni kumaanisha kwamba bilioni 1 216,4 zinazolingana na 62.4% ya bajeti yote zitatokea kazini za wananchi, bilioni 1071,6 zitapokewa kuhusu kodi pesa nyingine bilioni 110,8 zitapokewa kutoka njia nyingine ziwezekanazo.

Kuhusu fedha kutoka nchini Rwanda, Waziri Gatete amesema kwamba wenyebiashara watashauriwa kutumia mashini zitumikazo kwa kupelekea miswada kwa wateja zijulikanazo kwa jina la EBM (Electronic Billing Machine) kwa lugha ya kingeleza, ili kodi zipatikane kwa urahisi na kwa kiwango ambacho wanategemea kuhusu bajeti ya mwaka huu.


David Nzabonimpa.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments