Ubelgiji : Waziri wa mambo ya kigeni awasili Rwanda.

Katika safari ya siku nne ya kidiplomasia kandani la Afrika Mashariki, Waziri wa mambo ya nje wa Ubelgiji Didier Reynders baada ya kuzuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jumatatu, jumanne ya wiki hii, moja kwa moja ameendelea huku Rwanda.

Nchini Tanzania, Reynders alizungumza na Rais wa nchi hiyo Dk John Pombe Magufuli na viongozi mbalimbali ambapo walijadiliana hali ya maendeleo kisha aliziru hatua nyingi za maendeleo kama bandari ya Dar es salam, jengo la bunge ya Tanzania. Yeye pia alijadili hali ya kisiasa iliopo Burundi na Raisi mstaafu wa Tanzania William Benjamin Mkapa, mkapa.

Huku Rwanda, Reynders anatarajia kuanza safari ya siku mbili tangu leo mpaka alhamisi. Yeye atazungumza na baadhi ya viongozi, kuzuru makampuni ya wabelgiji, Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu, kutembelea Wabelgiji wanaoishi Rwanda mwishoni mwa ziara yake Reynders anatarajiwa kutembelea kituo cha kukumbuka waathirika wa mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Wa tutsi cha Gisozi.

Nchi ya Ubelgiji ndiye mhisani mipango ya nishati, hivi karibuni walitoa msaada wa milioni 55 dola za kimarekani kwa ajili ya kusambaza umeme katika kila kona za Rwanda.

Yeye aliyekuja Rwanda katika mwaka wa 2014 ambapo aliunga mkono Wanyarwanda kukumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 dhidi ya Watutsi kwa mara ya 20.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments