Rwanda kumuunga mkono mgombea wa Afrika, Dkt Adhanom.

Dk Adhanom Tedros Ghebreyesus
Mataifa mengi barani la Afrika hususan Rwanda wanaendelea kumuunga mkono Dkt Tedros Adhanon Ghebreyesus kuwa kiongozi wa shirika la Afya duniani WHO.

Dk Adhanom mwenye umri wa miaka 51 alikuwa waziri wa afya tangu mwaka wa 2005 hadi 2012 kabla ya kuchukua majukumu ya kuwa waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia, ikiwezekana akachagua, atakuwa Mwafrika wa kwanza kuongoza WHO.

Katika mkutano na wandishi wa habari jana, Waziri wa mambo ya kigeni na Ushirikiano pia msemaji wa Rwanda Bi. Louise Mushikiwabo ametangaza kwamba Adhanom ni mmoja miongoni mwa watu ambao wana uwezo wa kuongoza WHO.

Alisema ‘’tuna mgombea sahihi, tunadhani huu ni muda wa Afrika kuongoza tawi la afya la Umoja wa Mataifa.’’

Shirika la Afya ulimwenguni linalotarajiwa kuchagua kiongozi mpya atakayochukua nafasi ya Dk Margret Chan aliyekuwa kiongozi wa WHO tangu mwaka wa 2006 hadi sasa mwaka ujao. Adhanom alichagua kuwakilisha Afrika mwezi Januari na wakuu wa nchi za Afrika jijini Addis Abbaba.

Adhanom anagombania kiti cha uongozi wa WHO na Philipe Douste-Blazy, waziri wa zamani waAfya nchini ufaransa na Sania Nishtar ndiye aliyekuwa waziri wa Afya wa Pakistan.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments