Picha : Tiwa Savage rasmi ndani ya label ya Jay Z, Roc Nation

Jay Z, Tiwa Savage na Don Jazzy
Muimbaji wa Nigeria, Tiwa Savage amekuwa msanii mpya wa label ya Jay Z, Roc Nation.

Hatua hiyo imethibitisha tetesi hizo zilizoanza kusemwa kuanzia wiki mbili zilizopita kwa picha aliyoiweka Tiwa kwenye Instagram akiwa na bosi wake mpya Jay Z na yule wa sasa, Don Jazzy.

Tiwa Savage bado ni msanii wa Mavin Records ya Don Jazzy huku Roc Nation ikimsaini kwa ajili ya kumweka kwenye ramani ya kimataifa zaidi hususan Marekani.

Tiwa Savage na Don Jazzy walikutana na Jay Z kwenye makao makuu ya Roc Nation jijini New York Marekani.

Balozi huyo wa Forte Oil, MTN na Pepsi atakuwa msanii wa kwanza kutoka Nigeria kusainishwa kwenye label hiyo na kujiunga na Rihanna, Big Sean, DJ Khaled na wengine.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments