Waimbaji wa Abba wakutana baada ya miaka 30

Waimbaji wa Abba
Wanachama wanne wa bendi ya Abba wameonekana wakiwa pamoja nchini Sweden na kuwashangaza mashabiki kwa kuimba pamoja.

Nyota hao walikusanyika siku ya Jumapili katika warsha moja ya kibinafsi, kuadhimisha ushirikiano wa miaka 50 kati ya watunzi wa nyimbo Bjorn Ulvaeus na Benny Andersson.

Wakati wa warsha hiyo, Agnetha Faltskog na Anni-Frid Lyngstad waliimba wimbo "The Way Old Friends Do".

Baadaye Ulvaeus na Andersson walijiunga nao wakati walipokaribia kumaliza wimbo huo na kuwa ndiyo mara ya kwanza bendi hiyo kukutana na kuimba tangu miaka 30 iliyopita.

Wakati ilishuhudia mafanikio makubwa, bendi hiyo iliponea kuvunjika kwa ndoa kati ya Ulvaeus na Faltskog pamoja na Lyngstad na Andersson.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments