Tamasha la Mziki wa HIP-HOP nchini Rwanda.

Ukitoka kushoto Doplomate, Green P, Bac-T na P’fla
Kwa mara ya kwanza Rwanda inajiandaa kupokea bashi mkali wa midundo ya HIP-HOP itakayohudhuriwa na warapa watalaam zaidi kuliko wengine wa nchi ya milima mirefu Rwanda ndani ya ukumbi wa Romanz Regende Park paleeeee maeneo ya Rugende jijini Kigali.

Tamasha hii itawaleta pamoja Warapa kama Bull Dog aka BUDA, P’fla aka The Great, Green P aka ElGringo, Diplomate aka Deep G, Demo Crazy , Pacson na Yuleeee aliyezaliwa TZ mrapa Bac-T.

Hii Bang’i itafanyika siku ya jumamaosi tarehe ya 11, mwezi Juni mwaka huu tangu saa tisa za jioni mpaka Usiku.

Mwandalizi wa tamasha hilo Kajuga Robert alimbia Izuba rirashe kwamba warapa wamejianda na nguvu zaidi kwa kuwaapa burudani watu ambao watahudhuduria hii bashi. Aliongeza kwamba itakuwa tamasha ya mziki wa HIP-HOP tu na wasanii watakuwa warapa tu.

Bac T mmoja wa warapa watakayowawasha moto huko alisema kuwa atawapimia mashabiki misitari mikali ya kuwapeleka peponi ya Hip-hop.

Robert aliongeza kwamba DJ Africano atakuwepo kumix miziki ya HIP-HOP.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments