Mafunzo ya uokoaji katika maji yazinduliwa Kigali

Tangu tarehe 6 Juni 2016, Mafunzo ya uokoaji katika mahali ya maji yalianzishwa mjini Kigali, Ni mafunzi ambayo hutarajiwa kupunguza idadi ya vifo vya watu kadhaa ambao huzama katika maji. Haya ni masomo yanayohudhuriwa na watalaam 26 husika na usalama katika maji (Marines) kutoka nchi 9.

Brigadiani Jenerali. Safari Ferdinand mwakilishi wa Rwanda katika uzinduzi wa mafunzo haya, alisema “Lengo la mafunzo haya ni kuongeza uwezo wa walinda usalama katika maji kwenye nchi zinazopakana na bahari au ziwa ili wakati wa ajali waweze kuokoa watu wna kutafuta wale waliopotelea”.

Brig. Jen.Ferdinand

“Kuna ajali iliyotokea katika ziwa la Victoria, watu wengi waliaga dunia wengine walipotea kwa sababu ya kutokuwa na uwezo na elimu ya kutosha. Uwezo na elimu tunaowapa kwa sasa utatusaidia katika kupambana na ajali kama hizi”. Aliongeza.

Luteni Kanali S. K. Saeed kiongozi msaidizi wa shirika la EASF alisema “Ajali katika maji husababishwa na upepo. Wanapaswa kupima kasi na mwelekeo wa upepo hivi vinasaidi kujua watu hao hukaa wapi ili wawaokoe kwa uharaka na kupunguza vifo vya wengi”.

Luteni Kanali S. K. Saeed

Nchi zilizohudhuria mafunzo haya ni Rwanda, Uganda, Sudan, Kenya, Somalia, Ethiopia, Djibouti,Visiwa vya Komoro na Seyishele nchi ya Burundi pekee ndiyo hukutohudhuria mwaliko wa mafunzo hayo.

Mafunzo hayo yanatolewa na wataalamu kutoka ulaya nchi za Norway, Danmark na Sued.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments