Askari wa polisi ametumia risasi kwa kusitisha maandamano ya wanafunzi wa shule la sekondari Gicumbi.

Baadhi ya wanfunzi wameandamana huko Gicumbi kama video iliyosambazwa kwenye mtandao wa WatsApp inavyoonyesha.
Hii leo asubuhi tarehe 6 ya mwezi Juni Wanafunzi wa shule la Groupe Scolaire de Kageyo linalo makao katika tarafa la Kageyo , Wilayani Gicumbi, kasikazini mwa Rwanda wameandamana dhidi ya mshahara mdogo unaopewa walimu wao.

Anastase Kamizikunze, mkurugenzi wa shule hili ameambia mwanahabari wetu kwamba hawa walimu wameacha kazi baada ya kutoridhika na mishahara yao.

Mwandishi wa Redio Ishingiro inayofanyia kazi Gicumbi ametangaza kwamba hao wanafunzi wamevunja madirisha ya shule ambapo wanaposoma. kisha wakaenda mtaani wakipiga kelele. Akijaribu kusitisha hayo maandamano karao amepiga risasi juu kwa kujikingia kunyanyaswa na hao wadenti.

Waandamanaji ni wanafunzi wanaosadiwa kusoma na shirika la wakimbizi duniani (UNHCR), Wao wanasema kwamba hakufurahishwa na mshahara wanaosema kuwa duni sana kuliko wa walimu wanaofundisha wanafunzi wasio wakimbizi.

Mwanahabari ameendelea kusema kwamba sababu kuu iliyosababisha maandamano ni walimu wanaoishi kambini ya wahamiaji ya Gihembe wanaolipwa mshahara na mpango wa ADRA unaowapa mshahara duni kukilinganisha na walimu wanaolipwa na serikali.

Wakiandamana askari wa polisi aliyefika huko wanafunzi walijaribu kumrusha mawe kwa kujitetea alipaga risasi mbili juu . ingawa hadi sasa hakuna mmoja aliyesemwa kujeruhiwa.

Msemaji wa polisi katika jimbo la kasikazini Inspekta wa polisi Gasasira Innocent alithibitisha uwepo wa maandamano lakini alisema Yeye bado hakupokea habari kamili.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments