INATEK VC yatwaa kombe la GMT

INATEK VC na Sports S wa Uganda watwaa ubingwa wa shindano la mpira wa wavu lililolenga kukumbuka wanaspoti waliouawa katika mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka wa 1994 . Genocide Memorial Tournament ni shindano lililoandaliwa nchini Rwanda na shirika la mpira wa wavu kwa ushirikiano na kamati ya Olimpiki na Wizara ya michezo na utamaduni.

Shindando hilo lilianza tarehe 4 Juni 2016 timu zilianzia katika makundi, siku moja baadaye timu kutoka makundi mbalimbali ndizo zilizocheza nusu fainali. Kwa upande wa wanaume katika ½ timu ya Sports S (Uganda) ilishinda APR VC seti 3-2, INATEK VC ilifanya kazi ya ziada kwa kuifunga Nairobi Waters seti 3-0.

Sports S wanawake na wanaume wote baada ya kutinga fainali na baada ya Sports S ya wanawake kuibuka mabingwa baada ya kuichapa timu ya wanawake ya taasisi ya mapato Rwanda (RRA) seti 3-2, mashabiki walianza kusema kuwa wanaweza kushinda kwa pande zote mbili.

Lakini INATEK VC, timu iliyotoka chuoni cha kilimo na teknolojia mashariki mwa Rwanda iliwawonyesha kuwa ni timu chipukizi ya Rwanda ambapo iliwafunga kitalaam seti tatu kwa sufuri.

Timu zilizoshika nafasi ya kwanza zilipewa kombe na pesa laki mia tano (500) za kinyarwanda , timu ya pili ilipewa pesa laki mia tatu (300) za Kinyarwanda, ya tatu ilizawadiwa laki mia mbili.

Miaka miwili iliyopita, Rayon Sports VC ndiyo iliyoshinda mashindano haya maradufu lakini mwaka huu INATEK ndiyo timu iliyoibuka bingwa.

INATEK VC

Sports S

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments