CAF : Ndoto za kufuzu AFCON2017 zayeyuka.

Jana jumamosi katika nyasi za Amahoro, wanyarwanda walitegemea kusisismuliwa wikendi na timu ya taifa ya kandanda AMAVUBI lakini wakasikitishwa. Uwanjani Amohoro amavubi wa Rwanda walilambwa mabao 3-2.

Kala ya kuanza mechi, Rwanda walikuwa matumani kamili ya kuifunga Os Mamba wa Usumbiji. Lakini mwanzoni nohodha wa Wasumbilji Elias Gaspar Palembe ameshinda bao la Kwanza dakika ya 9 tu, 38 Jacqueas Tuyisenge amemjibu kwenye dakika ya 34 ambapo huyo mkali wa Rwanda ameandika goli la kusawazisha.

Wanyarwanda wameendelea kukabiliana na OS Mamba wa Usumbiji mpaka dakika ya 44 wakashindwa kutetea bendera ya nchi ambapo mchezaji chipukizi wa Usumbuji aitwa Apson David Manjate amewafunga bao la pili. Kipindi cha kwanza kimemalizika 1-2.

Katika pilikapilika za kipindi cha pili, katika dakika ya 77, Jacques Tuyisenge tena, huyo Tuyisenge anayeyichezea Gor mahia ya Kenya amepiga mkwaju hatari ana kwa ana akashinda bao la pili kwa upanda wa Rwanda. 2-2. bali nohodha machachari wa Usumbiji ameonyesha kivumbi wanyarwanda kwa kuwapiga kipigo cha lala salama kwenye dakika ya 78 [Rwanda 2-3Usumbiji].

Baada ya kunyakuliwa alama tatu za jana, Rwanda yakata tamaa kufuzu AFCON 2017 itakayofanyika kule Gabon. Hivi sasa Wao wanatazama nafasi katika mechi dhidi ya Ghana jijini Accra.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments