Wanajeshi 46 wahitimu masomo ya kulinda amani

Mwaka mmoja ndio wamesoma masomo hayo katika shule ya RDF Command and Staff College, mwanajeshi anayehitimu masomo haya ana elimu na uwezo wa hali ya juu katika kutawala na kuongoza wanajeshi katika nchi ama katika nchi za nje kulinda amani.

Msemaji wa majeshi ya Rwanda Luteni Kanali Rene Ngendahimana alisema “ Baadhi ya masomo wanayopewa yanahusu kuwa Afrika yaweza kuwa na uwezo wa kipekee wa kumaliza matatizo yanayoweza kuzuka bila kutegemea fimbo ya mbali”.

Meja Mutarambirwa ndiye aliyevunja rikodi katika masomo hayo, anaeleza kuwa katika mwaka mzima wamenufaika na kupata ujuzi wa ziada unaoungamana ujuzi waliokuwanao.

Mgeni rasmi waziri wa ulinzi Genarali James Kabarebe alisema “Ujuzi mliopata ni muhimu sana, nawaomba kufanya kwa bidii kuliko mlipofanya ili Afrika iendelee kusonga mbele mkitumia nguvu na uwezo wenu”.

Kwa mara ya nne wanajeshi wanapotimuza masomo RDF Command and Staff College. Wanajeshi 14 walitoka Burundi, Kenya, Tanzania, Sudani Kusini, Zambia na Malawi wengine 32 ni kutoka majeshi ya RDF.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments