Rwanda yaporomoka kwenye orodha ya FIFA.

Timu ya kabumbu ya Rwanda ’’AMAVUBI Stars’’ yaanguka chini nafasi 16 kwenye orodha inayotolewa kila mwezi na shirika la kandanda duniani ‘’FIFA’’.

Rwanda hivi sasa yakaa nafasi ya 103 kwenye orodha punde ya FIFA wakati mwezi jana ilikuwa kukaa nafasi ya 87.

Katika kanda ya Afrika mashariki, Jamhuri ya Demokrasia Congo imechukua nafasi ya 52, Uganda[72], Rwanda[103, Kenya[129], Burundi [132], Jamhuri ya Muungano wa Tanzania [136].

Barani Afrika Algeria imekuja ya kwanza[32], Côte d’Ivoire[36], Ghana [37], Senegali [41 ], Misri [45].

Ulimwenguni Argentina ni ya kwanza, Ubelgiji, Kolombia, Ujerumani, Chili, na Uhispania.

Rwanda imeporomoka baada ya kufungwa na Senegali katika mechi ya kirafiki mabao mawaili kwa sufuri uwanjani Amahoro jumamosi iliyopita (Mame Biram Diouf na Younousse).

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments