Ghasia nchini Syria, taswira ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi Rwanda – Jenerali Dallaire

Jenarali mstaafu Romeo Dallaire, Mkanada aliyekuwa kiongozi wa vikosi vya Umoja wa Mataifa Rwanda (MINUAR) katika miaka ya mauji ya kimbari dhidi ya Watutsi mwaka wa 1994 nchini Rwanda ni mojawapo wa kundi lililoonyesha picha 55,000 za Wasyria wanaoathiriwa na ghasia inayoendelea kujitokeza huko Syria.

Yeye aliambia wabunge wa Kanada kwamba vita inayoendelea kujitokeza Syria ni nakala ya Mauji ya Kimbari ya 1994 dhidi ya watutsi ingawaje nchi zenye nguvu hazitaki kuchangia msaada muhimu kwa kusitisha ghasia.

Runinga yiitwayo CCTV kule Kanada imetangaza kuwa katika mahojiano na wanahabari jumanne ya wiki hii, Dallaire alisema kwamba picha zilizokamatiwa nchini Syria zinaonyesha watoto, wanaume hata na wanawake bado wanaendelea kuawa kikatili.

Alisema ‘’kupitia masanamu, tulionyesha wabunge, Wakanada nini kinachoendelea kufanyika nchini Syria, Watu wanendelea kupoteza maisha kinyama katika vita bila sababu badala ya maridhiano.’’

Dallaire alisema kwamba Dunia inapaswa kusaini mapatano ya kusitisha vita haraka ; vita hadi sasa maelfu ya watu ambao walipoteza maisha na sasa mamilion watikuwa na makazi.

Romeo aliongeza kwamba Yeye mwenyewe alikondolea macho watoto wa makambi ya Jordan walipoingizwa katika kijeshi, ili ni taswira huo huo ya vilivyotokea Rwanda mwaka wa 1994. Miakani hiyo Dunia nzima hakukuwezi kuguswa dhidi ya hayo mauaji na sasa Ulimwengu hataki kufanya kitu cha kuwaokoa raia wa Syria, wanaangalia tu.

‘’ikiwa watu waanza kupata watoto kama majeda kwa sababu upumbafu hii ni lawama kwa Dunia nzima, tunapaswa kuwaokoa wananchi wa Syria.’’

Jenerali mstaafu Romeo Dallaire alikuwa kiongozi wa vikosi vya kulinda amani nchini Rwanda, Sasa ni mwakilishi wa taasisi inayolenga kutetea haki za kibinadamu na kuepuka mauaji ya kimbari.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments