Mikataba mitatu baina Rwanda na Uturuki yamesainiwa

Waziri wa mambo ya kigeni nchini Rwanda Louise Mushikiwabo na mwenzake wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu
Waziri wa mambo ya kigeni wa Uturuki na wa Louise Mushikiwabo walitia saini mapatano ya ushirikiano anaolenga kuimarisha elimu na kushirikiana kwa wizara hizo mbili za mambo ya nje na kurahisisha uhamiaji kati ya Rwanda na Uturuki kati kati ya Rwanda na Uturuki.

Tukio hilo limeandaliwa kwenye makao ya wizara ya mambo ya kigeni huko Kimihurura/Kigali, hapo ndipo waziri mkuu wa Uturuki Mevlüt Çavuşoğlu katika ziara yake aliongea na waziri wa mambo ya kigeni juu ya umoja na ushirikiano wa nchi hizo mbili.

Bw. Mevlüt alisema “ Bara la Afrika ni muhimu kwani lina vitu muhimu katika umoja na ushirikianao kwa nchi yetu, Rwanda ni mojawapo ya nchi muhimu kwa nchi yetu barani afrika, tunafurahi sana kuanzisha balozi yetu hapa Kigali na Accra (Ghana)".

Aliendelea kusema “ Tunashukuru kwa fahamu mliyotujalia na kukubali kampuni yetu ijenge Kigali Convention center itakayopokea mkutano wa umoja wa afrika. Tunataka Rwanda isonge mbele ikiongozwa rais Kagame, tunatumaini kuwa nchi hii itaendelea kusonga mbele kwenye ngazi zote".

Mawaziri wote wamekubaliana kushirikiana kwa makampuni ya ndege Turkish Airway na Rwanda Air kwa kurahisisha safari kati ya Rwanda na Uturuki.

Waziri wa mambo ya kigeni Louise Mushikiwabo alisema “ Kuna bahati ya wafanyabiashara wa Uturuki na Rwanda, makampuni ya Uturuki yameanza kufanyia kazi nchini Rwanda katika idara ya kuzalisha nishati. Wafanyabiashara wa Uturuki ni watalaam tutachora somo muhimu kutoka kwao, tunatazama fursa ndani ya uchumi, uganga na ujenzi".

Mawaziri hawa walipomaliza kusaini walienda kuzindua balozi ya Uturuki nchini Rwanda, hivi vitarahisisha huduma kwani makao ya balozi ya Uturuki yalikuwa nchini Kenya.

Jengo la Ubalozi wa Utururki

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments