Green Party yailalamikia serikali Mfalme Kigeli V arudi Rwanda

1

Green Party ni chama pekee kinachosema kuwa hakikubaliani na serikali ya Rwanda hivi wengi wameviona wakati serikali ilipotaka kubadilisha katiba kwa mahitaji ya wananchi hapo ndipo chama hicho kilipeleka serikali mbele ya mahama makuu kwa kusema kuwa hivyo ni kinyume na katiba.

Chama cha Green Party kimeomba serikali ya Rwanda kufanya iwezekanavyo ili Mfalme Kigali V Ndahindurwa mwenye umri wa miaka 80 kuhamia uhamishoni huko Marekani.

Kiongozi wa chama hiki Dkt Frank Habineza alisema “ Kuna muda mrefu uliopita tukisikia kuwa anataka kurudi. Habari tuliyosikia ni kuwa amekataa kurudi kama mtu wa kawaida na rais Kagame alitaka mfalme arudi lakini havikuwezekani pia kuna wengine ambao walihitaji arudi lakini vimekuwa tatizo kubwa”.

Msemaji wa ofisi ya Kigeli V Ndahindurwa, Boniface Benzige alivyosema “ Mfalme hataki kurudi kwa siri, anahitaji jamii ya wanyarwanda ijue kurudi kwake nchini alimozaliwa, hawezi kuchukuliwa kama mtu wa kawaida”.

Muda mrefu umepita serikali ikiomba arudie nchini haya hudhihiririshwa na maneno ya rais Kagame aliyoyasema kuwa itakuwa bora zaidi kwani serikali imemuomba kutoka uhamishoni kama wanyarwanda wengine wanaokuja kutoka mataifa mengine.

Tatizo ni kujua atakuja lini, ingawa atakuja kama mfalme ama kama mnyarwanda wa kawaida, lakini akija itakuwa bora kwake.

Rwanda ni nchi inayoongozwa na katibu yaani si nchi ya kifalme kutoka 1961 hii inamaana ya kuwa Kigeli V wakati anaporudi hawezi kuwa na kuishi kama mfalme isipokuwa kubadilisha sheria za sasa.

Serikali imefanya iwezekanavyo ili arudi nyumbani ingawa Green Party husema “hawezi kuchaguliwa mahitaji yake, anaweza kupewa kama sheria inavyosema yeye aliongoza nchi na kupewa mali zake alizonyang’anywa ambazo hukaa Nyanza”.

Wanasheria wanasema kuwa hivi ni kinyume cha katiba kwani mfalme hakubaliwi kupewa nafasi ya heshima ama kuwa seneta kama Green Party inavyosema. Mali zinazokaa Nyanza si za mtu binafsi yaani ni za serikali.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. Nchi za rwanda na burundi zinafaa kuongozwa nawa falme kwasababu tangia uflme utolewe nchi hizo hakuna amani kabisa nanadhani hatakwuwepo hata sikumoja !!

Tumia Comments