Sababu ya kutofanya collabo na mkenya, Danny afunguka

Mrapa Danny Nanone ametangaza kuwa wakati alipoenda Kenya alikuwa na mpango wa kutafuta msani kutoka Kenya ili wafanye collabo lakini hivi havikuwezekana kwa sababu ya mipango aliyokuwa nayo.

Mwanzoni mwaka huu 2016 msanii huyo Danny Nanone alizindua mpango wake wa daftari inayo ujumbe wa maonyo kwa vijana.

Katika mahojiano na Makuruki.rw Danny Nanone alitangaza kuwa baada ya kuenda Kenya katika mpango wake wa kufanya madaftari, alijaribu kuiga mziki wa Kenya na kutafuta msanii wa kufanya collabo naye lakini kwa sababu ya muda mfupi havikuwezekani.

Alisema “Nilipofika Nairobi nilitazama jinsi mziki unavyofanywa na kuhitaji msanii wa kushirikiana naye lakini havikuwezekani kwani havikuwepo katika mpango wangu, sikuweka nguvu katika mpango huo kwani nilikuwa na muda mfupi ndio maana niliamua kurudia mwangu”.

Danny Nanone anasema kuwa anaheshimu kufanya collabo na msanii wa nchi nyingine kwani ni njia rahisi ya kuvunja rekodi na kuvuma katika nchi hiyo ya msanii mzalendo.

Danny Nanone ni mmoja ya wasanii wanaopigania shindano la Primus Guma Guma Super Star kwa mara ya sita.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments