Rusizi : Zawadi ya Rais Kagame yaanza kupotea

Wakati Rais Paul Kagame akawatembelea wanachi wa Rusizi, katika jimbo la magharibi mwa Rwanda, Yeye aliwazawadi meli ya kusafiri watu ili wapate kipato kutokana na safari za meli hiyo. lakini hivi sasa chombo hicho kinasemwa kuwa kiwango cha faida waliotegemea kimeanza kupunguka.

Meli hii hufanya safari tarehe 16 mwezi Mechi,2016 kutoka Rusizi, Karongi, Rutsiro hadi Rubavu, mavuno walipatao kabla yamepunguka kwa kiasi kikubwa sana.

Kankindi Léoncie anayeshughulikia masuala ya kiuchumi huko Rusizi pia mhasibu wa meli hii ametangaza kuwa hawafaidiki kama zamani.

Alisema “ Upotevu na upunguaji wa mvuno, Mimi sikuoni tofauti. kwani tunapotuma wafanyakazi kutafuta pesa tukaona kuwa pesa zimepunguka ukilinganisha na hali ya zamani ni ishara ya upunguaji wa mavuno”.

Barabona Evaritse ni mwanaraia alisema “ Hawatuambii mavuno kutoka meli hii kwa kila mwaka ili tulinganishe na tujue utofauti kati ya miaka hiyo na kujua ingawa tumefaidika, ni meli inayopata pesa na tunahitaji pesa hizo zitumike kwa ajili ya wananchi wasiojiweza, walipiwe mituelle de santé na watoto walipiwe ada ya shule”.

Mwaka jana familia mia moja kutoka Nkombo zimepewa mbuzi kutoka mavuno ya meli hii pia wamekubaliwa meli ndogo itakayowasidia kuvuka ziwa la Kivu kutoka mavuno ya meli hii kubwa.

Meli hii hukutana na tatizo kubwa uharibifu na kusababisha kutofanya muda mrefu na kuna meli iliyokuja kufanya safari katika ziwa la Kivu ndiyo sababu kubwa ya hasara hiyo.

Wafanyakazi wa meli hii wanasema kuwa zamani walipata pesa milioni moja kwa kila safari ya kuenda na kurudi, lakini leo hupata laki mia tatu. Safari kutoka Rusizi hadi Rubavu ni elfu sita mia tano za pesa.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments