Uzamukunda aka Baby, Nirisarike Salomon kukosa michuano ya CAF

Uzamukunda Elias aka Baby
Mshambuliaji nyota wa timu ya soka wa Rwanda Uzamukunda Elias aka Baby anayechezea Le Mans ya Ufaransa katika daraja la tano pamoja na Bonge la beki Nirisarike Salomon anayechezea Saint-trond wamethibitishwa kuwa hawatakucheza dhidi ya Msumbiji tarehe 4 mwezi Juni,2016 kwa kusaka tiketi ya kufuzu kombe la bara la Afrika CAN/2017 huko Gabon.

Meneja wa timu ya taifa , Bonnie Mugabe aliambia magazeti kwamba Babay atakosa mechi ya Msumbiji kutokana na jeraha la goti .

Yeye alijeruhiwa wakati akifanya mazoezi ya mwisho baada ya kujiunga na Amavubi, Mugabe amesema kuwa nyota huo bado hakupona.

Kuhusu sakata ya Solomon, Mugabe amesema yaani Salomon hatakushughulikia mechi hii kutokana na tatizo la nyaraka zake za usafiri.

Jumamosi/tarehe ya 28 mwezi Mei mwaka huu, Rwanda ilifungwa mabao 2-0 na Senegal kwenye nyasi za Amahoro. Rwanda vs Msumbiji tarehe 4 Juni,2016 itakuwa mechi ya kufa na kupona , Rwanda ikagonga kisika itakosa tiketi.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments