Mji wa Kigali wakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari didhi ya watutsi

1

Tarehe 27 Mei 2016, wafanyakazi na viongozi wa mji wa Kigali walikumbuka waliokuwa wafanyakazi na viongozi wa mji huu ambao waliuawa katika mauaji ya kimbari didhi ya watutsi.

Tukio hilo lilianza baada ya kuzuru jingo la makumbusho ya mauaji ya kimbari didhi ya watutsi hapo Gisozi, wafanyakazi, viongozi na familia za waathirika waliweka maua kwenye kaburi kwa lengo la kuwapa heshima waliovunjiwa na wauaji.

Dusabemungu Gervais ambaye alikuwa kiongozi wa mji wa Kigali alionyesha ushiriki wa Renzaho Tharcisse na Karera Francois wote walihukumiwa kwa sababu ya ushiriki katika mauaji ya kimbari didhi ya watutsi

Alisema “Renzaho aliagiza vyakula nje ya nchi na kusema kuwa wanyarwanda wanaumwa na njaa na kuagiza vinywaji kutoka Bralirwa lakini vilitumiwa na interahamwe”.

Mukaruliza Monique meya wa mji wa Kigali alisema “ Mauaji ya kimbari yalipangwa na kuwekwa matendoni kwa sababu ya uongozi mbaya lakini tunajua yalisimamishwa mashujaa ya wanyarwanda ambao walikataa ubaguzi".

Aliendelea na kusema kuwa Rwanda ina usalama na kuheshimiwa kwenye ngazi za kimataifa kwa ajili ya uongozi usiobagua na kutetea umoja na ushirikiano wa wanyarwanda hapo ndipo anahamasisha wanyarwanda kupiga marufuku wale wanaotetea itikadi ya mauaji ya kimbari didhi ya watutsi.

Mgeni rasmi, makamu rais wa seneti Jeanne D’ Arc Gakuba alisema “ Ningependa wadogo watege masiko kwa makini kwani mtu anaamka mapema akaona mataa yanamlika, akaona ujenzi wa jingo unatimizwa na kudhani kuwa hayo yote yanakuja kwa urahisi lakini vitu sivyo hivyo. Mnapaswa kujua ushujaa na mikakati iliyowekwa ili tuwe na umoja wa wanyarwanda na haki ya kila mtu”.

Uongozi wa mji wa Kigali unaomba mtu yeyote ajuae habari za watu waliokuwa wafanyakazi wa mji wa Kigali ambao waliuawa katika mauaji ya kimbari ili idadi kamili ijulikane.

Viongozi mbalimbali

Jeanne d’Arc Gakuba (kushoto) na Mukaruliza Monique

wafanyakazi wa mji wa Kigali

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments