Binti wa rais Kagame, Ange Kagame amehitimu masomo yake

1

Ange Ingabire Kagame, binti ya Paul Kagame rais wa Rwanda amehitimu masomo yake katika chuo kikuu cha Smith College, Massachusetts nchini Marekani.

Sherehe hizo zilifanyika mwishoni mwa wiki jana, baadaye Ange Kagame alionyesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa Facebook maneno yafuatayo . “Siku ya Jana ilikuwa ya furaha mimi na rafiki zangu.” Aliandika.

Alionekana katika sare za wanafunzi waliohitimu masomo yao, akiwa pamoja na wanafunzi wenzake waliohitimu masomo yao mwaka huu. Ange alifuatilia masomo ya siasa alijikuwa akijikita pia kuhusu historia ya bara la Afrika.

Mara nyingi alikuwa akihudhuria mikutano ya kimataifa kuhusu elimu, haki za wanawake na mengineyo.

Ange Kagame ni mtoto wa pili kati ya watoto wanne wa rais Kagame. Alizaliwa mwaka wa 1993, na ndiye msichana pekee wa rais Kagame.

Ferdinand Maniraguha

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

Tumia Comments