Kamonyi : Mwenye umri wa miaka 75 na mjukuu wake wanahangaikia usalama wao

Mzee mwenye umri wa miaka 75 apaaza sauti kwa kupigwa mawe na watu wasiojulikana ambao hutupa juu ya paa, Licha ya ujulikanao wa tatizo lake katika uongozi.

Sindambiwe Paul wa kujiji cha Rugara, tarafa ya Musambira, Mkoani kusini mwa Rwanda anasema kuwa paa ya nyumba yake imeharibika kwa sababu ya mawe hutupwa juu paa na watu bado hakutambulika.

Babu huyu anasema kuwa tatizo hilo si la kipekee kwani na mjukuu wake Musabyimana Jean Marie Vianney ana tatizo hilo.

Sindambiwe anasema kuwa katika mkutano wa kijiji uliofanywa mwezi Aprili wallijadiliana tatizo hilo na kumuahidi usalama lakini katika usiku wa tarehe 22 na 23 Mei wahusika wa kitendo hicho cha upotofu walirudia kama kawaida.

Alisema “ Tatizo hilo tumeliambia uongozi na kupanga ulinzi lakini kutoka usiku wa jumanne walirudia tena kitendo chao cha kutupa mawe juu ya nyumba yangu, kwa sasa niko kama mtu anaeishi nje kwani paa imeharibika".

Katika mahojiano na Makuuruki.rw katibu mtendaji wa kiiji cha Cyambwe, Barongerwa Elysee alisema “ Tunajua tatizo hilo labda linaweza kutokana na matatizo ya familia kwani mzee huyu ana matatizo ya mashamba na familia yake”.

Kiongozi huyu anasema kuwa mhusika wa kitendo hicho hajakamatwa ili alipe mali zilizoharibika lakini anampa moyo mzee huyo kwani punde si punde wanaenda kutafuta suluhisho la tatizo hilo.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments