Kocha mkuu wa AS Muhanga awapa moyo mashabiki

Kocha aliyepewa majukumu kwa sasa kwenye timu ya AS Muhanga Abdou Mbarushimana ana mzigo wa kuokoa timu hii ambayo inakuja kwenye nafasa za mwisho katika mashindano ya ligi kuu, alisema kuwa hakuja kufanya maajabu lakini matatizo aliopitiamo atamsaidia kuokoa timu hii.

Tarehe 23 Mei 2016 ndipo uongozi wa AS Muhanga ulisema kuwa kocha Mbarushimana Abdou aliyekuwa kocha wa Rayon Sports ndiye kocha anayeajiriwa na timu hii ambayo iko matatani hapo ni baada ya masaa machache yakuonyeshwa mlango kwa kocha Rutayisire Edourd na wasaidizi wake.

Katika mahojiano na Ntivuguruzwa Severin kiongozi msaidizi wa timu hii, amekubali habari hii kwamba Mbarushimana amepewa majukumu ya kuzoesha na kuokoa timu hii.

Alisema “ Ni ukweli tumempa kazi kocha Mbarushimana ili atatusaidie katika mechi zinazobaki ili tuweze kusonga mbele na kubaki katika ligi kuu”.

Kiongozi huyu anasema kuwa kocha Rutayisire alionyeshwa mlango kwa sababu ya tabia zake potofu.

Kocha mpya wa timu hii Mbarushimana Abdou alisema “ Nilikuwa nikishiriki katika soka, AS Muhanga walinisogelea kwa lengo la kuisaidia timu hii naona kuwa hali ya sasa ya timu hii ni sawa na hali kama yangu ya wakati uliopita, tunataka kufanya na kupata alama za kutosha. Tukishuka katika daraja la pili tutajaribu kufanya kwani sikuja kufanya maajabu lakini tutashirikiana”.

Hakuna bahati ya kubaki katika ligi kuu kwani AS Muhanga iko tatika nafasi ya mwisho na alama 14 na Rwamagana inayokuja kwenye nafasi ya 15 ambayo inaizidi alama 9.

Hivi vinaonyesha kuwa AS Muhanga inatarajiwa kushinda mechi zote ili iwe na matumaini ya kubaki katika ligi kuu.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments