Kwa nini Ufaransa huchelewesha kuhukumia wahusika wa mauaji ya halaiki ?

Uongozi wa IBUKA unasema kuwa kuna sababu nchi tofauti zinazofanya Ufaransa kuchelewesha kesi za wahusika wa mauaji ya kimbari didhi ya watutsi, ya kwanza ni kuwa wanataka kuficha wahusika kwani waliwasaidia na kuwa washahidi waage dunia kabla ya kutoa ushahidi au wasahau.

Wakati MIFOTRA, MINALOC na MININTER walipokumbuka wahanga waliofanyia mawizara yaliotajwa juu, kiongozi msaidizi wa IBUKA Nkuranga Egide alionyesha kidole cha shahada nchi ya Ufaransa kuendeleza itikadi ya mauaji ya kimbari didhi ya watutsi kwani katika hukumu ya Octavien na Tito Barahira walionyesha watu filamu inayoendeleza itikadi ya mauaji ya kimbari jina maarufu la Rwanda’s Untold Story.

Alisema “ Kuna sababu tatu zinazosababisha nchi kuchelewesha hukumu. Kwanza wanataka kuficha wale walioshiriki katika mauaji ya kimbari, pili ni kutoonyesha ushiriki wao katika mauaji ya kimbari, tatu ni kuchelesha muda ili washahidi wazeeke kabla ya kutoa ushahidi au wasahau".

Aliomba wanyarwanda wote kushirikiana na kujiunga nguvu ili waonyeshe ukweli kuhusu mauaji ya kimbari yaani kutoa ushahidi au pesa ili washiriki wa mauaji ya kimbari wahukumiwe.

Kwa sasa mfaransa Alain Gautier na mkewe walianzisha shirika aliloita Collectifs des Parties Civile Pour le Rwanda kwa lengo la kutafuta ishara za watu wanaohukumiwa nchi Ufaransa ambao walishiriki katika mauaji ya kimbari na shirikisho hilo linasaidiwa na shirikisho la wanyarwanda liitwalo Amis des Collectifs des Parties Civile Pour le Rwanda.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments