Mazungumzo ya amani ya Burundi yaanza Arusha

Rais Mstaafu wa Tanzania Benjamin Mkapa
Mazungumzo ya amani ya kutatua mgogoro wa kisiasa nchini Burundi yameanza jijini ARUSHA kwa makundi mbalimbali kukutana chini ya uenyekiti wa Rais Mstaafu Benjamin Mkapa

Akifungua majadiliano hayo Mzee Mkapa amesema ili kuleta amani nchini Burundi kinachotakiwa ni Burundi kutatua mgogoro huo wenyewe kwa kwenyewe.
Amesema ni vema kutoa nafasi kwa wadau kutoa maoni yao na njia za kufanya jambo ambalo litahusisha makundi mbali mbali ikiwemo vyama vya siasa nchini Burundi pamoja na asasi za kiraia.

Rais mstaafu Mkapa amesema ana imani na jumuiya za kimataifa na marafiki wataendelea kusaidia hatua za kurejesha nchi ya Burundi katika hali ya kawaida ili wananchi waendelee na shughuli za kuongeza uchumi.

Amesema amefurahishwa na jitihada za Umoja wa Mataifa,Umoja wa Afrika pamoja na Jumuiya ya Kimataifa kwa kuhakikisha kuwa mazungumzo hayo ya Burundi yanafanyika vizuri.

Katika mkutano huo serikali ya Burundi imewakilishwa na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki nchini Burundi na Waziri wa Mambo ya Ndani na Nje.

Katibu Mkuu wa Chama cha CNDD,Willium Munyema Mbabazi, ameomba makundi yote yanayohusika na mgogoro huo yashirikishwe ili kupatikana kwa amani ya kudumu.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments