Mashindano ya Big Brother Africa yavunjwa

Kama ulikuwa unasubiria kuona mashindano ya Big Brother Africa basi pole sana sababu kwa mwaka huu hayatakuwepo.

Mashindano ya Big Brother yametokea kuwavutia watu wengi kutokana na kukutanisha washiriki wanaotoka mataifa mbalimbali ya Afrila, huku Tanzania ikionekana kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Taarifa zilizotolewa na waandaaji wa mashindano hayo kupitia M-Net wamesema kwa sasa wanajiandaa kuweka mikakati ili kuboresha mashindano hayo hapo mwakani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments