Rwanda kutumia ‘’Zipline drones’’ kwa kusambaza damu nchini kote.

Waziri wa afiya nchini Rwanda Dkt. Agnes Binagwaho amesema kwamba ndege ziitwazo” Zipline drones” katika lugha ya kingeleza zitatumiwa kuharakisha usambazaji wa damu katika maeneo mbalimbali nchini na kupunguza uhalibifu wa damu.

Bi. Binagwaho amesema kuwa ndege hizi zitatumika kwa kuleta damu kwenye zahanati 45 kwa ujumla, kila ndege yaweza kubeba kilogram 1.5 ; Kwa mwanzo, Mradi utaanzishwa kwenye kliniki 21 tangu mwishoni wa 2016, Badaye zahanati 45 kamili.

Amesema kwamba mtambo mrefu ndege hizi zatuumia kwa mahili mbali ni dakika 45 . Hii ni jibu la swala Rwanda ilikuwa nalo la kupoteza damu nyingi zikiharibu na idadi kubwa ya wagonjwa waliopoteza roho kwakukosa damu zahanatini.

Bi. Binagwaho amesema kwamba nchini Rwanda kuna mahali pili au tatu zinazokusanya damu. Ilikuwa hatali kuleta damu kwa kila zahanati. Lakini ndege hizi zitatusaidia.

Ameongeza kwamba watu huwa na damu tofauti. Ili mtu apone, kila zahanati ilipaswa kuwa na kila aina ya damu. Lakini kuanzia mwishoni mwa mwaka huu ndege zitatumiwa kwa kuleta damu mahali popote.

Amesema ‘’damu ni muhimu sana kwa maisha ya kila mtu. Miaka iliopita waliharibu 6% ya damu yote. Lakini ndege hizi zitatuwezesha kupunguza idadi ya mahali pakuwekea damu nchini Rwanda.’’

‘’Kila zahanati nchini Rwanda ina damu. Lakini ajali inawapasa kuagiza damu nyingine kutoka zahanati nyingine za mbali. Ndege hizi zitatumiwa kuleta damu ili wagonjwa wasipoteze maisha.’’ameongeza

Hodari wa matumizi ya damu katika baraza la afya nchini Rwanda RBC, amewaambia watangazaji kwamba si rahisi kuchunga damu kwa joto kila aina ya damu inayohitaji.

Rwanda ndiyo nchi ya kwanza barani Afrika inayotumia ndege kwa kubeba damu kwenye zahanati. Rwanda itapewa ndege hizi na Zipline kutoka nchi ya Marekani.

Vimeshathibitishwa kuwa watu kutoka Zipline watakuwa hapa nchini Rwanda mwezi Julai mwaka huu. Watakuja kusawazisha mambo yote baada ya kuleta ndege hizo. Mwezi wa Novemba, baina ndege 12 kwa 15 zitaanza kazi katika zahanati 21 nchini Rwanda.

David Nzabonimpa

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments