Msichana wa Chibok kukutana na Rais Buhari

Habari kutoka BBC inasema kuwa Msemaji wa Serikali ya Nigeria amesema msichana kutoka Chibok, aliyeokolewa hivi karibuni kutoka mikononi mwa Wanamgambo wa Boko Haram, atakutana na Rais Muhammadu Buhari na kupata msaada wa kuweza kuchangamana na jamii yake.

Aliachiwa huru akiwa na mtoto mchanga, hili ni tukio la uokoaji la kwanza kwa kipindi cha zaidi ya miaka miwili.

Zaidi ya wasichana mia mbili walitekwa na kundi hilo la Boko haram mwezi April mwaka 2014.

Jeshi la Nigeria limesema tayari limeshamkamata Mohammed Hayatu mfuasi wa Boko Haram ambaye inasemakana ni mume wa msichana huyo. Zaidi ya wasichana mia mbili walitekwa na kundi hilo la Boko haram mwezi April mwaka 2014.

Msemaji wa serikali ya Nigeria Garba Shehu ameiambia BBC kuwa msichana huyo wa Chibok, aliyeokolewa hivi karibuni kutoka katika mikono Boko haramu atakutana na Rais Muhammadu Buhari na atapewa msaada na serikali ili aweze kurejea katika jamii.

Naye Aboku Gaji ambaye ni kiongozi wa kikundi cha wanamgambo ambaye alimuokoa binti huyo na kuiambia BBC juu ya namna familia yake ilivyompokea aliporudishwa nyumbani.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments