Kigali kuguswa dhidi ya tatizo la Trafiki Jam.

Ukitembea daima mjini kwenye masaa ya Asubuhi, mchana na jioni huchelewa kufika nyumbani au kazi kwani umecheleweshwa na msongamano hatari wa magari barabarani. Kwa hiyo sababu na nyingine hutesa watumiaji wa barabara, Uongozi unapanga suluhisho kupitia mpango wa BRT (Bus Rapid Transit).

Katika mahojiano maalum na Makuruki.rw, Mjibika wa miundombinu katika uongozi wa mji wa Kigali Bw. Reuben Ahimbisibwe amefunguka kuwa mji ulianza kupanga suluhisho linalojulikana kwenye jina la BRT linalotegemeka kurahisisha usafiri.

Asema kuwa wakaenda kuchagua mabarabara kutumika na mabasi ya watu kwa uwingi. Ahimbisibwe asema kwamba walenga kuokoa muda unaopotea wakati abiria wangojea mabasi. Pia wanataraja kutumia Simu ya mkononi kwa kutraki wapi basi imefika.

Akasema ’’tutachagua mabarabara sahihi ambao abiria wanatumia kwa uwingi, kwani mabasi ya abiria na magari kibinafsi katika huo barabara, ndiye sababu kubwa inasababisha trafiki jam ; pia teknolojia yatatumika kwa kuwezesha watu kujua wapi basi ipo kabala ya kuondoka nyumbani.’’

Mpango huu utaanza kwenye line ya mabasi Kigali-Remera, Kigali-Kabeza, Kigali-Kanombe, Nyabugogo-Nyamirambo Hata ikiwa tarehe ya mwanzo bado hakujulikana, Ahimbisibwe aeleza kwamba Uongozi wa Kigali yataka kuharakisha huyu mradi.

Janvier KARANGWA

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments